Karibu kwenye Base Swahili Blogs.
Fahamu Base ndiyo blockchain au mnyororo mkubwa wa Layer-2 wa Coinbase, ambao umepata umaarufu mkubwa ndani ya jumuiya ya Web3 kutokana na mfumo wake rahisi kutumia na ushirikiano na makampuni makubwa kimataifa.
Katika mwongozo huu utajifunza kuhusu blockchain au mnyororo wa L2 wa Coinbase na namna unayofanya kazi.
Base blockchain ni nini?
Fahamu mnyororo wa base, ulitengenezwa na kampuni kubwa ya ubadilishaji wa crypto inayofahamika kama coinbase, ni suluhisho la mnyororo wa Layer-2 linalotumia faida za OP Stack kutoka Optimism. Base inaleta makato ya mihamala karibu sifuri na kwa haraka na usalama uliothibitishwa na nguvu ya Ethereum.
Coinbase inafanya jitahidi za kukuza mnyororo wa base ikitumia uzoefu wa miaka zaidi ya kumi katika kutengeneza bidhaa za crypto. Hata hivyo, base inahitaji kujitegemea baada ya muda.
Base inalenga kuwapa watumiaji wake uhuru usio na vizuizi pamoja na uwazi kwa yeyote. Base imejengwa kwa kutumia OP Stack, na kwa hivyo ipo kwenye superchain modular, optimistic rollup agnostic. Wazo ni kwamba minyororo yote iliyojengwa kwa kutumia OP Stack inaweza kutuma mali kwa urahisi kati yao bila vikwazo vikubwa.
Mnyororo wa Base unafanyaje kazi?
Base ni optimistic rollup, inayotumia OP Stack. Rollups huchakata miamala nje ya mnyororo kwa makundi, kupunguza gharama za miamala na kupunguza msongamano kwenye mtandao. Kwa kutumia OP Stack, miamala huunganishwa ili kupunguza gharama. Utaratibu huu unatekelezwa kwenye mainnet ya Base, lakini hukamilishwa kwenye mainnet ya Ethereum. Kwa hivyo, Base hutumia usalama wa mnyororo wa Ethereum.
Kama optimistic rollups nyingine, Base huchukulia kuwa muamala ni halali. Hii inamaanisha kwamba hesabu za ziada hazihitajiki mwanzoni. Hata hivyo, mfumo utaendesha uthibitisho wa udanganyifu kuthibitisha muamala wa kutiliwa shaka. Njia hii inapunguza gharama.
MWISHO
Jiunge nasi kwa kusubscribe kwenye blog ya Base Swahili ili upate taarifa kuhusu base pamoja na fursa zinazopatikana kwenye teknolojia ya crypto, blockchain. Usikose! Tembelea blog yetu sasa na uwe sehemu ya jamii yetu. #BaseSwahili
Dr Joshua